Katika
pita pita zangu huku bondeni, nimegundua kitu kimoja, wabongo jamani
wameloea huku.. mh mpaka najiskia aibu...ukitembea tu kidogo..
unakisikia kiswahili kileee cha nyumbani.. wengi wanakaa tu kwenye
vigenge na kupiga story zisizo na maana.. najiuliza swali.. sasa kama
familia kule nyumbani zinawategemea; ndugu na jamaa wanasema kwamba
kijana wetu bwana yuko kule ng'ambo akitafuta maisha na atatusaidia...
kijana mwenyewe ndiye huyu ninayemuona hapa ambae kweli hata
kujishughulisha, hajishughulishi...inakuweje? yaani natamani
ningewakalisha semina miwape somo moja hilo! mbaya zaidi ninaambiwa
nisije nikathubutu kufikiri kwamba wabongo wote marafiki zangu.. ndiyo
siku kila nlichokibeba kitatolewa mikononi mwangu na maisha yangu kuwa
hatarini.. mh kweli Mungu atusaidie... mara nyingi tunaisema serikali
yetu na kuilaumu lakini kwa hawa huku je? inabidi tubadilishe mawazo
yetu.. tuache fikra duni na hasi tufanye kazi kwa bidii na kuacha uvivu
na ulegevu. badiliko linaanza na wewe...
No comments:
Post a Comment